Wednesday, 15 July 2020
Monday, 25 May 2020
Kuripoti chuoni tarehe 30/5/2020
CHUO CHA UALIMU MOROGORO
MAELEKEZO MUHIMU KWA WANACHUO
Kutokana na maelekezo ya Serikali ya kuwa Vyuo vifunguliwe tarehe 01/06/2020 kwasababu ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.Hivyo, wanachuo wote wanatakiwa kuripoti Chuoni tarehe 30/5/2020 ili ufundishaji na ujifunzaji darasani uanze rasmi tarehe 01/06/2020.
Kila mwanachuo atatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
a) Uwe na Kitakasa Mikono (Sanitizer) kwa matumizi yako binafsi ili kujilinda na kuwalinda wengine.
b) Uwe na Barakoa utakazozitumia pindi ukiwa kwenye mikusanyiko ya watu.
c) Ufikapo chuoni, unatakiwa kujisajili getini na katika ofisi ya Usajili ambako utapewa maelekezo muhimu ya namna ya kuishi salama hapa chuoni.
d) Kuzingatia taratibu na tahadhari zote zilizowekwa na Wizara ya Afya katika safari yako na kuishi kwako hapa chuoni.
Karibu tena chuoni na ninawatakia safari njema ya kurejea chuoni.
AUGUSTINE J. SAHILI
MKUU WA CHUO
Tarehe 25/05/2020
Wednesday, 25 March 2020
MOTCO !!! EVERYWHERE AND ANYTIME
| |MAKTABA TETEA-ACSE)| |
| |MAKTABA TETEA- DSEE| |
| |*****COMPUTER SCIENCE| |
Subscribe to:
Posts (Atom)